Raia wa Ghana wanaelekea kwenye uchaguzi mkuu hii leo kumchagua rais mpya na wabunge.
Wachunguzi wanakadiria kuwa ushindani utakuwa
mkubwa kati ya rais wa sasa John Dramani Mahama na Nana Akufo-Addo,
ambaye babake aliliongoza taifa hilo katika miaka ya sabini.Duru zinasema kuwa ushindani utakuwa mkali sana hasa baada ya bwana Akufo-Addo kufanya vyema katika uchaguzi uliopita.
Wapiga kura wametumia mitandao ya kijamii kutoa uhamasisho kuhusu uchaguzi wa amani na huku wengi wakielezea kuwa na hamasa kubwa
Ghana kwa miaka mingi imekuwa kipenzi cha waekezaji katika eneo ambalo lenye historai ya migogoro ya kisiasa na hata mapinduzi.
Moja ya mada inayojadiliwa miongoni mwa wapiga kura imekuwa mapato yanayotakana na mafuta na ambavyo nchi inaweza kuyatumia vyema.
Rais wa sasa bwana Mahama, ameahidi kuboresha viwango vya maisha katika nchi hiyo ambayo raia wa kipato cha chini hupata chini ya dola nne kwa siku.
Mpinzani wake bwana Akufo-Addo, anayeunga mkono soko huru, ameahidi kutumia mapato yanayotokana na mafuta kuendeleza sekta ya elimu.
No comments:
Post a Comment