Shirika la
kimataifa linalopinga rushwa linasema rushwa bado ipo kwa wingi katika
nchi zilizozipindua serikali zao katika harakati za mapinduzi ya kiraia
yaliyofanyika katika nchi za kiarabu.
Utafiti wa shirika hilo kuhusu jinsi rushwa
inavyopokewa kimataifa na ndani ya sekta za umma, pia umetaja kuwepo
matatizo katika nchi zinazoitumia sarafu ya euro zilizoathirika na mzozo
wa kiuchumi.Na ripoti hii inaashiria kuwa nchi za kiarabu na za mashariki ya kati ambazo hivi karibuni zimeshuhudia mapinduzi bado zinakabiliwa na wakati mgumu kulidhibiti tatizo hili.
Kwa jumla rushwa katika nchi zinazoitumia sarafu ya euro ni kidogo kuliko katika eneo la mashariki mwa Ulaya, lakini shirika la Transparency International linasema kutokana na mzozo wa kifedha, serikali zinapaswa kujitahidi kuimarisha taasisi za uma na kuongeza uwajibikaji.
Utafiti huo unajumuisha zaidi ya nchi mia moja na sabini na Uingereza inajaribu kusalia katika nchi ishirini zilizo juu ya orodha.
No comments:
Post a Comment