Nchini Japan chama cha kimuhafidhiin cha Liberal Democratic, LDP, kinaelekea kushinda kwa viti vingi katika uchaguzi mkuu.
Huo ni ushindi mkubwa kwa chama kilichoshindwa vibaya na chama cha mrengo wa kushoto katika uchaguzi uliopita.
Ni miaka mitatu tu tangu wapigaji kura wa Japani kukitoa madarakani chama cha LDP kilichotawala kwa miaka mingi, na kukumbatia chama cha Democrat.
Lakini leo wapigaji kura wamebadili maoni - wamekipa kura nyingi sana chama cha LDP na kukirejesha madarakani.
Waziri Mkuu atakuwa Shinzo Abe, mwanasiasa wa mrengo wa kulia.
Ameahidi kuwa atachukua msimamo mkali dhidi ya Uchina na atapenda kubadilisha katiba ya Japani, ambayo hairuhusu Japan kuingia katika shughuli za kivita.
Hatua hizo zitaungwa mkono na chama kipya cha Japan Restoration.
Chama hicho kimefanya uzuri na kinaweza kuwa na viti kama 60 kwenye bunge jipya.
Kama walivotabiri wengi, Japan imebadilisha msimamo na kuelekea kulia.
No comments:
Post a Comment