Sunday, June 9, 2013

Host wa tuzo hizo mwaka huu alikuwa ni Zembwela na TJ.
Hii ni list nzima ya tuzo hizo.

Wimbo bora wa mwaka

Dear God – Kala Jeremiah

Msanii bora wa Kiume
Diamond

Msanii bora wa kike
Lady Jaydee

Msanii bora wa kike Taarab
Isha Mashauzi

Msanii bora wa kiume Taarab
Mzee Yusuf

Msanii bora wa kiume Bongo Flava
Diamond

Msanii bora wa kike Bongo Flava
Recho

Msanii bora wa Hip Hop
Kala Jeremiah

Msanii bora wa kiume Bendi

Chalz Baba

Msanii bora wa kike Bendi
Luiza Mbutu

Msanii bora anayechipukia
Ally Nipishe


Video bora ya mwaka
Baadaye – Ommy Dimpoz

Mtunzi bora wa mashairi Taarab
Mzee Yusuf

Mtunzi bora wa mashairi Bongo Flava
Ben Pol

Mtunzi bora wa mashairi hip hop
Kala Jeremiah

Mtunzi bora wa mashairi Bendi
Chalz Baba

Mtayarishaji bora wa mashairi muziki wa kizazi kipya
Man Walter

Mtayarishaji wa wimbo wa mwaka – Taarab
Enrico

Mtayarishaji wa wimbo mwaka – Bendi
Amoroso

Mtayarishaji chipukizi wa mwaka
Mesen Selekta

Rapper bora wa bendi

Fagasoni

Wimbo bora wenye vionjo vya asili

Chocheeni Kuni – Mrisho Mpoto ft Ditto

Wimbo bora wa bendi

Risasi Kidole – Mashujaa Band

Wimbo bora wa Reggae

Kilimanjaro – Warriors from The East

Wimbo bora wa Afrika Mashariki
Valu Valu – Jose Chameleone

Wimbo bora wa Bongo Pop
Me an You – Ommy Dimpoz ft Vanessa Mdee

Wimbo bora wa kushirikiana/Kushirikishwa
Me and You – Ommy Dimpoz ft Vanessa Mdee

Wimbo bora wa Hip Hop
Nasema Nao – Nay wa Mitego

Wimbo bora wa rnb

Kuwa na Subira – Rama Dee ft. Mapacha

Wimbo bora wa ragga/ dancehall
Predator – Dabo

Wimbo bora wa Taarab
Mjini Chuo Kikuu – Khadija Kopa

Wimbo bora wa zouk rhumba

Ni wewe – Amini

Bendi bora ya mwaka

Mashujaa Band

Kikundi bora cha Taarab
Jahazi Modern Taarab

Kikundi bora cha muziki wa Kizazi kipya
Jambo Squad

Hall of Fame – Institution

Kilimanjaro Band wana Njenje

KWANINI DIAMOND KAVAA HIVI ?.


DIAMOND

CHINI  NI  LIST YA WATU MAARUFU KUTOKA KENYA NA TANZANIA, AMBAO WAMETAJWA NA MTANDAO WA KENYA KUA NI MAFREEMASONS | WACHAFUZI WA MAJINA YA WATU

Inawezekana kila kitu kina wakati wake, kuna muda watu walikuwa wakisikia neno ‘Freemason’ ama ‘Illuminate’ kama inavyojulikana nchini Kenya wengi walikuwa wanaiona ni habari kubwa, lakini kwa sasa hivi inaweza kuchukuliwa kama sio big deal.

Sababu ni ile ile kuwa wengi wanaoendelea kwa haraka ama kuwa juu katika kile wanachokifanya basi utasikia huyo ni member wa Freemason, kwa upande wa Marekani wanasema ‘he/she just sold her/his soul to the devil’. 

Japo kwa upande wa Marekani wapo wanaokiri kufanya hivyo kweli, ila kwa Africa Mashariki hakuna msanii aliyewahi kukiri.

Lakini yote hayo ni kama yanakanganya na kuonekana kama hayana mantiki hasa pale ambapo vithibitisho vya kinachoongelewa huwa havileti mantiki ya moja kwa moja.

Pengine watu wanatafuta pesa kwa bidii na kumuomba Mungu lakini kwa kuwa kwenye mstari wa juu wanajikuta wanahisiwa kuwa member wa secret society (Freemason). Oh..au labda ndo vile kwa upande mwingine lisemalo lipo na kama halipo laja !

Tunathubutu kuziita blaa blaa kwa upande mwingine, lakini tukiweka kwenye mabano kuwa inaweza kuwa na ukweli, who knows!

Mtandao wa malimwengu wa nchini Kenya huenda ukawa na mfano mzuri wa kile nilichokitaja hapo juu, mtandao huo kupitia mwandishi wake imetaja majina ya wasanii wa Tanzania na Kenya wanaosemekana kuwa ni wafuasi wa Freemason, lakini kizuri zaidi ni kwamba mtandao huo umejaribu kuonesha vithibitisho na kushindwa kupata jibu la moja kwa moja kwa nini wasanii hawa wamekumbwa na hili.

Inabaki hivyo hivyo kuwa tetesi tu.
Hawa ni wasanii waliotajwa na maelezo yanayowahusu:
Kutoka Tanzania


1.Naseeb Abdul Jumaa (Diamond Platinum)
Picha aliyopiga mwaka jana akiwa na mzungu anaeaminika kuwa ni moja kati ya viongozi wa Freemason wakiwa wameweka pozi na kuonesha ishara inayooaminika kuwa ni ya Freemason, na kwamba alipoulizwa yeye alisema hakufahamu kama alikuwa anaelekezwa kupiga picha kwa pozi la ki-freemason. Kwa mujibu wa mwandishi anaona inaweza kuwa kweli kwa sababu anaonekana kuenjoy! 

2.Ali Kiba




Iliwahi kusemekana pia kuwa Ali Kiba ni Freemason, na wewe pia unaweza kufikiria sababu kwamba eti alikuwa maarufu sana na baadae kufifia. Maoni ya mwandishi (Hakuna uthibithibisho/ushaidi unaoweza kuwekwa thidi yake).
   

3.Jacquelin Wolper

Ni muigizaji maarufu wa kike mtanzania. Maoni ya mwandishi ( Hakuna ushaidi, tetesi peke yake hazina umuhimu)

KENYA:

1.Camp Mulla

Maoni ya mwandishi (Hapana, sio kweli. Sababu ya kufanikiwa kwenye muziki haimaanishi kuwa ni members wa Freemason. Hakuna mtu mwenye ushahidi kuwa Camp Mulla ni members wa Freemason).

2.Octopizzo
Maelezo yanayomhusu yanaonekana kuwa mengi sana kama kawaida, ni moja kati ya wasanii ambao tetesi za kuwa illuminate ni nyingi zaidi.

3.Nonini
Ukimtaja Nonini kama Illuminati lazima kitu serious zaidi kiandikwe ama ikielezwe.
Nonini sio Illuminati (maoni ya mwandishi).


Hao ndio waliandikwa na kutolewa maoni ama maelezo na muandishi wa mtandao huo. Lakini tetesi huwa nyingi na kuongezeka mara kwa mara kwani hata Avril pia huwa anatajwa kuwa Illuminati na kwamba kazi yake ni kueneza usagaji nchini humo na eti sababu mojawapo ni mashairi ya wimbo wake ‘Chokoza’.

Haya yote yanasemwa tu, cha kufanya ni kile alichokisema Prof. Jay kwenye wimbo wake ‘Bongo Dar es Salaam’... 

 “Akili kumkichwa, ukizubaa unaachwa feri”.

HABARI KWA HISANI YA http://kiwale11.blogspot.com

PICHA ZA KILICHOJIRI KATIKA BIRTHDAY YA LULU


5 comments:

  1. Happy birthday LULU and many more years to come I wish you all the best and success in your life and GOD protect you.All the best Take care.
    Reply
  2. uko sawa dada..happy b.day..hope ur getting better not older
    Reply
  3. ilikuwa poa happy birthdai
    Reply
  4. punguza kujipamba wewe ni mrembo hata bila hizo makeup nyingi unazozikandika.
    Reply
  5. it so Nice to see lulu, finally out of problems after all.god this powefully.we o happy for dear!!!
    Reply

TAZAMA JINSI WASHINDI WA TUZO HIZO ZA KILIMANJARO TANZANIA MUSIC AWARDS 2013. WALIVYOJINYAKULIA TUZO HUKU KALA JEREMIAH NA OMMY DIMPOZI WAKIONGOZA

MTUNZI BORA WA MASHAHIRI HIP HOP-KALA JEREMIAH
WIMBO BORA WA KUSHIRIKIANA;OMMY DIMPOZ ft VANESSA-ME AND YOU
MTUNZI BORA WA MASHAHIRI -BENDI; CHARLS BABA


                    WIMBO BORA WA RNB; RAMA DEE ft MAPACHA-KUWA NA SUBIRA

                                KIKUNDI BORA CHA TAARABU-JAHAZI MODERN TAARAB

MTUNZI BORA WA TAARABU-THABIT ABDUL

WIMBO BORA WA TAARABU;KHADIJA KOPA-MJINI CHUO KIKUU

MTAYARISHAJI WA WIMBO WA MWAKA KWA TAARABU-ENRICO

                                       MSANII BORA WA KIKE -TAARBU; ISHA MASHAUZI


                                       MTUNZI BORA WA MASHAHIRI BONGO FLAVA-BEN POL



                             MSANII BORA WA KIUME BONGO FLAVA-DIAMOND

                                    MSANII BORA WA KIKE BONGO FLAVA-RECHO


KIKUNDI BORA CHA MUZIKI WA KIZAZI KIPYA-JAMBO SQUAD
MTAYARISHAJI CHIPUKIZI WA MWAKA-MENSEN SELECTA
MSANII BORA WA KIKE-BENDI ;LUIZA MBUTU
WIMBO BORA WA ZOUK; AMINI -NI WEWE





Mwaka huu umekuwa mwaka mzuri zaidi kimuziki kwa msanii toka rock City Mwanza Kala Jeremiaha ambae maombi yake kwa ‘Dear God’ yamesikika na amepata majibu kwa njia ya kipekee na wimbo wake ‘Dear God’ umeweza kuchukua tuzo tatu katika Kilimanjaro Music Awards 2013.  
 
Kala Jeremiah ametumia mkuki mmoja kunasa ‘swala’ wake watatu muhimu mwaka huu, Dear God imeweza kumpa nafasi kubwa na kushinda tuzo katika kipengele cha wimbo bora wa Hip Hop.



Nguvu ya wimbo huo hapana shaka ndiyo imemuwezesha pia kuondoka na tuzo ya msanii bora wa Hip Hop na Mtunzi bora wa mashairi ya Hip Hop.

Kala aliweza kuwapenya wasanii wazito kama Fid Q, Joh Makini, Mwana FA, Profesa Jay na mdogo wake katika game Stamina wa Moro Town waliokutana nae katika vipengele vya Hip Hop.

Wimbo huu ulitengenezwa na mtayarishaji chipukizi Dee Classic ambae pia alikuwa anawania tuzo katika kipengele cha mtayarishaji chipukizi wa Mwaka lakini hakuweza kushinda tuzo hiyo ambayo ilienda kwa Mesen Selector.
Msanii mwingine wa bongo fleva aliyeng’ara katika tuzo hizo ni Ommy Dimpoz ambae pia aliondoka na Tuzo tatu, ambazo ni Video bora ya wimbo bora ya mwaka, wimbo bora wa Bongo Pop ‘Me and You’ akiwa na Vannessa Mdee ambao pia uliwapa tuzo ya wimbo bora wa kushirikishwa/kushirikiana.

Wasanii na watayarishaji wa muziki wa bongo fleva ambao kwa mara ya kwanza wameweza kujishindia tuzo za Kili ni pamoja na kundi la Jambo Squared toka Arusha (Kundi bora la muziki wa kizazi kipya), Rama Dee ‘Kinega’ (Wimbo bora wa RnB ‘Kuwa na subira).

Wengine ni Amini (Wimbo bora wa Zouk Rhumba ‘Ni wewe’), Recho (Msanii bora wa kike Bongo fleva), na Nay wa Mitego (Wimbo bora wa Hip Hop ‘Nasema Nao’). Mesen Selecter (Mtayarishaji chipukizi wa Mwaka), Ali Nipishe (Msanii bora anaechipukia).

Tuzo hizo zimeshuhudiwa huku mfalme na malkia wa muziki wa kibongo wakitangazwa kuwa Lady Jay Dee ‘Anaconda’ (Msanii bora wa Kike) na Diamond Platinumz (Msanii bora wa kiume).

Friday, June 7, 2013

MAJAMBAZI YALIYOVAA NGUO KA WANAWAKE YAUAWA WAKATI YAKIJARIBU KUIBA.



WATU wawili wanaosadikiwa kuwa majambazi waliokuwa wamevaa kikekike wameuawa na wananchi wenye hasira kali baada ya kuwakurupusha wakivunja duka usiku. 


Mauaji hayo yalitokea eneo la Nyegezi Kijiweni, Kata ya Mkolani, wilayani Nyamagana jijini Mwanza, majira ya usiku, Mei 29, mwaka huu wakiwa katika harak

ati za kuvunja maduka matatu yaliyopo eneo hilo.

Watu hao ambao ni wanaume wanadaiwa siku ya tukio wakiwa na silaha ya moto (bunduki) walivunja nyumba tatu na duka moja katika eneo hilo kwa kutumia vifaa mbalimbali vya jadi.


Imedaiwa kuwa wakati majambazi hayo manne yakifanya uhalifu huo, mawili yalivaa makoti meusi marefu na yaliyobaki yalijitanda ushungi na kujifunga kanga na kujipaka wanja usoni ili yasitambuliwe.


Chanzo hicho kilieleza kuwa majambazi wawili waliokuwa na silaha ya moto, baada ya kukurupushwa walikimbia na kutokomea kusikojulikana.


Wananchi kuona hivyo waliwadhibiti waliovaa mavazi ya kike na kuwashambulia kwa kuwakatakata kwa mapanga hadi kuwaua. 


 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Naibu Kamishna (DCP) Ernest Mangu (picha ndogo), alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa uchunguzi unaendelea.

MALKIA WA TAARAB HADIJA KOPA AFIWA NA MUMEWE LEO


 Jafari Ally enzi za uhai wake akiwa na mkewe Malkia wa Mipasho nchini Tanzania, Khadija Omar Kopa wakifuatilia onesho la Mshauzi Classic ndani ya Mango Garden. 
Habari zilizoufiki mtandao huu hivi punde zinasema kuwa Kijana mtanashati aliyekuwa Mume wa Malkia wa Mipasho nchini, Khadija Kopa, aliyefahamika kwa jina la Jafari Ally, amefariki dunia leo alfajiri katika Hospitali ya Lugalo jijini Dar es Salaam, alikokuwa amelazwa akitibia kile kilichoelezwa alikuwa akisumbuliwa na kifua. 

Jafari na Khadija Kopa, walifunga ndoa mwaka 2008.
 Wakati kifo hicho kinatokea mke wake hakuwepo jijini Dar, kwani alikuwa safarini Rukwa alikokwenda na kundi zima la TOT kwa ajili ya kusherehesha Sherehe za Siku ya Mazingira Duniani zilizofanyika Kitaifa mkoani humo, ambapo leo anatarajia kuwasili jijini. 

Ratiba kamili ya msiba huo bado hadi sasa haijafahamika lakini inadhaniwa huenda msiba huo ukawa  maeneo ya Chaline au Lugoba ambako ni nyumbani kwa wazazi wa Marehemu.

USHIRIKI DARFUR MIKONONI MWA SERIKALI- TENGA

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Tenga amesema kuwa ushiriki wa klabu za Tanzania kwenye mashindano ya Kombe la Kagame yaliyopangwa kufanyika kwenye miji ya Darfur Kaskazini na Gordofan Kusini nchini Sudan unategemea tamko la Serikali ambayo kwa sasa inafanya tathmini ya hali ya usalama.
Tenga, ambaye alikuwa akizungumza na waandishi wa habari kwenye ofisi za TFF, alisema tayari TFF na Serikali zimeshafanya mazungumzo, na Serikali imepewa taarifa zote muhimu kuhusu mashindano kwa ujumla, malazi ya klabu za Tanzania, uhakika wa usalama, usafiri wa ndani na mambo mengine muhimu hivyo kwa sasa Serikali inatathmini taarifa hizo kabla ya kutoa tamko.
“Masuala ya usalama yako nje ya uwezo wa CECAFA. Kwa hiyo, kama Serikali itabaini kuwa hali usalama ya huko si nzuri, hatutaziruhusu na kama ikiona hali ni nzuri, itaruhusu,” alisema Tenga.
“Jukumu la CECAFA (Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu vya Nchi za Afrika Mashariki na Kati) ni kuandaa mashindano na kupata uhakika wa usalama kutoka nchi mwenyeji.
“Kama tukipata uhakika huo wa usalama, mashindano yanafanyika. Lakini nchi moja moja zinayo haki ya kuhoji usalama kwa kuwa ni wajibu wa Serikali hizo kujali maisha ya wananchi wake.”
Tenga alisema kuwa mashindano hayo yalikuwa yafanyike Ethiopia, lakini katika dakika za mwisho nchi hiyo iliomba isiandae mashindano hayo hadi mwakani na ndipo Sudan ilipojitokeza kuokoa mashindano hayo.
Alisema wakati wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Kimataifa la Vyama vya Mpira wa Miguu (FIFA) uliofanyika Mauritius, CECAFA iliitisha mkutano mkuu wa dharura na kupewa taarifa ya maandalizi ya mashindano hayo kutoka uongozi wa Chama cha Mpira wa Miguu cha Sudan na wanachama wakaridhia baada ya kuhakikishiwa usalama.
“Hivyo nchi wanachama wa CECAFA zimeridhia kushiriki baada ya kuhakikishiwa usalama, lakini kwa kuwa Waziri wetu ameonyesha wasiwasi kuhusu usalama wa Darfur, hatuna la kufanya zaidi ya kumsikiliza. Ni kauli ya kiongozi anayeonekana kuwajibika na ni lazima tusubiri tamko la Serikali,” alisema Tenga.
“Lakini napenda kuishukuru Serikali ya Sudan kwa uamuzi huo kwa sababu kuandaa mashindano hayo si kitu kidogo. Tayari Katibu Mkuu wa CECAFA (Nicholas Musonye) ameshakwenda kwenye maeneo hayo na kukaa wiki nzima akikagua viwanja na hoteli zitakazotumika na kuridhika nazo,” alisema.
Alisema watu wasipotoshe tamko la Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe alilolitoa Bungeni kuhusu ushiriki wa timu zetu Darfur.
“Mhe. Membe alisema Serikali itafanya uchunguzi ijihakikishie kuwa hali ya usalama ni nzuri… alisema Serikali haitakubali kuruhusu raia wake kwenda Darfur wakati hali ya usalama si nzuri,” alisema Tenga.
“Kwa maana hiyo, na baada ya TFF kuipa Serikali taarifa zote muhimu kuhusu hali itakavyokuwa wakati wa mashindano, sasa tunasubiri tamko la Serikali. Na hii ni kawaida kabisa kwa kuwa hata hapa tunapoaandaa mashindano, ni lazima kwanza tupata uhakika wa usalama kutoka serikalini ndipo tuziite timu.”
Alifafanua kuwa si jukumu la CECAFA kuamua mashindano yafanyike mji gani na kwamba chama cha nchi mwenyeji ndicho kinachoamua mashindano yafanyike mji gani.
“Sasa kwa suala la Sudan, magavana wa majimbo hayo mawili ya Darfur Kaskazini na Gordofan Kusini waliomba kwa chama chao mashindano hayo yafanyike kwenye miji hiyo na Serikali ya Sudan ikaihakikishia CECAFA usalama,” alisema.

“Sasa ikitokea Serikali yetu ikasema hali si nzuri, hatutaziruhusu timu zetu ziende kwa sababu masuala ya usalama yako nje ya CECAFA.”
TAIFA STARS SASA INAJITOSHELEZA- TENGA
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeishukuru Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kwa kuiwezesha timu ya taifa, Taifa Stars kuondokana na matatizo na kuwaomba Watanzania kuiombea timu ili ifanye vizuri katika mechi yake ya kesho (Juni 8 mwaka huu) dhidi ya Morocco mjini Marrakech.
Stars, ambayo inashika nafasi ya pili kwenye kundi lake la mashindano ya awali ya Kombe la Dunia ikiwa nyuma ya Ivory Coast kwa tofauti ya pointi moja, inacheza na Morocco katika mechi ya nne itakayofanyika Marrakech baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 katika mechi ya kwanza iliyofanyika Dar es Salaam mwezi Machi.
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Rais wa TFF, Leodegar Tenga alisema kuwa tangu kuanza kwa udhamini, TFF haijawahi kupata udhamini mkubwa kama wa Kilimanjaro Premium Lager ambayo imeingia mkataba wa miaka mitano wa kuidhamini Stars wenye thamani ya dola milioni 10 za Marekani.
“Katika kipindi chote hiki hatujawahi kupata udhamini ambao umekidhi mahitaji yote ya timu kama huu wa TBL,” alisema Tenga kwenye mkutano na waandishi uliofanyika kwenye ofisi za TFF.
“Lakini katika mwaka mmoja uliopita (tangu TBL ianze kudhamini) hatujawahi kushindwa kuisafirisha timu; kushindwa kulipa posho za wachezaji; kutanguliza watu wetu kwenda nje kuiandalia timu sehemu nzuri; kuzilipia tiketi za ndege timu tunazocheza nazo mechi za kirafiki na hata kuzilipia ada ya kucheza mechi (appearance fee).
“Posho za wachezaji zimepanda kwa karibu mara mbili na ndio maana leo wachezaji wanaijali timu yao. Yote haya ni kutokana na udhamini huu. Watu wanasema usione vinaelea….”
Tenga alisema kuwa udhamini huo ndio sasa umeanza kuzaa matunda na timu inafanya vizuri ikiwa ni pamoja na kuwa na maandalizi ya muda mrefu.
“Sasa tunawaomba Watanzania waiombee timu na tunawashukuru wale waliokwenda Morocco kuishangilia kwa kuwa vijana wetu wanapata nguvu pale wanapoona kuna watu wako nyuma yao,” alisema Tenga.
Rais huyo wa TFF pia alisifu kitendo cha Rais Jakaya Kikwete kuiita timu Ikulu na kuongea na kula na wachezaji, akisema kitendo hicho kitasaidia kuongeza hamasa kwenye timu.
Naye Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe alisema kampuni yake itaendelea kuwa bega kwa bega na TFF na kwamba uhusiano baina ya pande hizo mbili umeimarika na utaendelea kuimarika.
Katika mkutano huo, Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) lilikabidhi fulana maalum kwa ajili ya mashabiki ambao wamekwenda Morocco kuishangilia timu.
Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa NSSF, Juma Kintu alisema tayari fulana 250 zimegawiwa kwa mashabiki walioko Morocco na nyingine zilitarajiwa kusafirishwa jana.

MWILI WA MUME WA MALKIA WA MIPASHO YA TAARAB, KHADIJA KOPA KUZIKWA MUDA HUU BAGAMOYO.


Wakazi wa mtaa wa Magomeni wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa mum
e wa Khadija Kopa, Jafary Ally ambaye ni Diwani wa CCM kata ya Magomeni wakati wakielekea makaburi kwa ajili ya shughuli za mazishi.
Picha kwa hisani ya mdau Said Swala Iddy.

MSHIRIKI WA BBA KUTOKA TANZANIA FEZA KESSY ANAHITAJI KURA ZENU WATANZANIA ILI AWEZE KUENDELEA KUBAKI MJENGONI.JINSI PIGIA KURA SOMA ZAIDI HAPA




MPIGIE KURA FEZA JAMANI KWANI KURA YAKO NDIYO ITAKAYOMFANYA ASITOKE KATIKA BIG BROTHER THE CHASE. KESHO KUTWA
KWA KUTUMIA SIMU YAKO YA MKONONI
TUMA SMS NDANI YA SMS ANDIKA VOTE FEZA
VODACOM - 15456

ZANTEL - 15456

AIRTEL - 15456

TIGO - 15456

HAWANI NI BAADHI YA WATU MAARUFU WALIOJITOKEZA MAZISHI YA ALBERT KENETH MANGWEA JAMHURI MKOANI MOROGORO.


P-FUNK a.k.a MAJANI KUSHOTO NA MHE MBUNGE WA MBEYA MJINI, JOSEPH MBILINYI a.k.a SUGA WAKIBADILISH
ANA MAWAZO MARA BAADA YA MHE MBUNGE KUWASILI KATIKA UWANJA WA JAMHURI MOROGORO NA WAFUATIA NI BAADHI YA WASANII WA MUZIKI WA KIZAZI KIPYA NCHINI TANZANIA.

 JOHN MAKINI
 T.I.D
 MB DOGG
 JUMA KASSIM NA KUNDI LAKE AKIINGIA JAMHURI.
 AFANDE SELA KULIA NA BONDIA FRANCIS CHEKA (SMG)
 PROFESA JAY KUSHOTO NA T.I.D
 HUYU NDIYE WEMA SEPETU NDANI YA UWANJA WA JAMHURI.
MC KOBA KULIA AKISALIMIANA NA KAKA YAKE FID Q.