Monday, April 1, 2013

RIPOTI YA MAKONGO HIGH SCHOOL KUHUSU KUFELI KWA DOGO JANJA, MATOKEO NA MAHUDHURI


Baada ya taarifa kuenea kuhusu uwepo wa msanii Dogo Janja nchini Afrika Kusini kwa show alizopata zilizofanyika ndani ya wiki tatu, Uongozi wa shule anayosoma ya Makongo Sekondari, umetoa taarifa kuhusu mwenendo wake pamoja na matokeo aliyopata ya kidato cha pili.
Michael Alfred Mbaula ambae ni Afisa taaluma amesema “mahudhurio ya Dogo Janja darasani yalikua mazuri na alikua anashirikiana vizuri na wenzake kipindi kilichopita ila mara yake ya mwisho kuingia darasani ni novemba 2012, na kwa sasa atalazimika kurudia kidato cha pili kwa sababu amefeli kwa wastani mdogo ambao usingemruhusu kuendelea na kidato cha tatu”
Kuhusu kauli ya Dogo Janja kwamba juzi alipokwenda Afrika Kusini alikua ameomba ruhusa ya wiki mbili shuleni, Mbaula amesema “sio kweli kwamba aliomba ruhusa na wala ofisi haina taarifa japo shule haina tatizo akitoa taarifa hata katikati ya masomo iwapo anatakiwa kufanya shughuli za mziki kwa sababu Makongo ni shule ya vipaji, kuomba ruhusa ya wiki moja au mbili ambazo alikua akiziomba mwaka uliopita ndani ya mwezi mmoja ni sahihi ila kukaa miezi mitatu bila kuja shule ndio tatizo”
Katika sentensi nyingine, Mbaula anasema “Dogo Janja amefeli kidato cha pili kwa kupata wastani wa 27 ambapo alifanya vibaya sana kwenye hesabu kwa kupata sifuri, Civics alipata 27, historia 33, Jiografia 22, Kiswahili 46, Kiiingereza 42, Phisics 20, Chemistry 30, Biology 27, Commerce 8, Bookkeeping 11 hivyo ni lazima arudie darasa kitu ambacho anaweza kukifanya hapahapa Makongo”

HAYA NDIO MAGAZETI YA LEO MAR 31 2013, MICHEZO NA HARDNEWS.

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
DSC03438
.
.
.
.
.
.

Monday, March 11, 2013

MWENYEKITI WA JUKWAA LA WAHARIRI ABSALOM KIBANDA AVAMIWA,AJERUHIWA VIBAYA KICHWANI NA WATU WASIOJULIKANA

image
Pichani ni Ndugu Absalom Kibanda akiwa amelazwa kwenye moja ya chumba cha matibabu,hospitali ya Taifa Muhimbili.Get Well soon Absalom Kibanda.Picha kwa hisani ya Mtandao wa Mabadiliko.
Mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri,na Mhariri Mkuu wa Mtendaji wa New Habari Coperations Ltd, Ndugu Absalom Kibanda, amevamiwa usiku  wa kuamikia leo akiwa anashuka nyumbani kwake Mbezi Beach na watu wasiofahamika na kumpiga kichwani. Amepata majeraha Makubwa kichwani na hasa jichoni,aidha taarifa inaeleza kuwa baada tukio hilo Kibanda alikimbizwa hospitali ya Taifa Muhimbili kwa Matibabu.
Wadau hii ni taarifa ya kushtua sana,lakini tutazidi kutaarifiana kadiri ya habari zitakavyokuwa zinapatikana,kikubwa tumwombee Mungu amponye haraka mpiganaji mwenzetu.

VB CODE

Private Sub Timedisplay_Timer()
Dim Today As Variant
Today = Now
lblDay.Caption = Format(Today, "dddd")
lblMonth.Caption = Format(Today, "mmmm")
lblYear.Caption = Format(Today, "yyyy")
lblNumber.Caption = Format(Today, "d")
lblTime.Caption = Format(Today, "hh:mm:ss ampm")
End Sub

Monday, January 7, 2013

SENTENSI 5 ZA ROMA MKATOLIKI KUHUSU UHUSIANO WAKE NA KUNDI LA KINA JOH MAKINI.

Roma Mkatoliki.
Rapper Roma Mkatoliki ambae ni mzaliwa wa 96.0 Tanga ameitii kiu ya mashabiki wengi wa hip hop waliotaka kujua siku akifungua kinywa chake kuhusu kundi la WEUSI atasema nini.
Kwenye Exclusive interview na millardayo.com Roma amejibu maswali machache mazito kuhusu WEUSI ambao wengi waliamini kama ana beef nao.
Wakati akiizungumzia single yake mpya ya 2030 Roma alitumia hiyo nafasi pia kuweka wazi kwamba haba beef wala chuki na kundi la Weusi na kama vile haitoshi akatolea mfano status aliyoiandika kwenye page yake ya facebook siku kadhaa kabla ya kuwasifia WEUSI kwa show yao ya mwaka pale Maisha Club.
Joh Makini na Nikki wa II siku ya show december 23 2012.
Japo anasema baada ya kuiandika hiyo status kuna ambao walimuunga mkono na waliompinga, namkariri akisema “kuna waelewa na wasio waelewa… mara nyingi tumfatilishe yule muelewa, kitu kikiwa kizuri mimi ni mtu wa kukubali, ndio hivyo nilivyoumbwa haiwi kwa njia ya unafiki au kwa kutafuta kitu kingine chochote, ile show ya WEUSI ilikua kali mi Maisha Club nakwenda sana kwenye show nyingi lakini ilikua ni show nzuri jinsi ilivyopangiliwa, haikupata watu wengi sana kama nilivyotarajia lakini hata waliofika inatosha, kikubwa nilichokipenda ni show ambayo haikumuhusisha msanii mwingine yeyote… walifanya show nzuri kuanzia Lord Eyez, Nikki, Bonta, G alitisha sana Joe mwenyewe alifanya vizuri, haikuniboa hata kidogo”
“Jana yake usiku kabla ya show nilikua nao kina Lord na G nikapiga nao stori lakini once wanapofanya mistake kwenye game unagundua hapa wamekosea hilo pia sitalifumbia macho nitaweza kuliongea, kama unakuta 50 na Jay Z wanabeef lakini tunashangaa 50 anapoperform Jay Z anaamka kwenye kiti kabisa anapiga makofi anaonekana ana mzuka, mawazo ya watu tu kwamba labda watu wakiwa na utofauti basi siwezi kukubali mtu akifanya vizuri, mbali na hivyo vyote nilivyoviongea hakuna matatizo kati ya Roma na wale watu, najiona niko sawa sina matatizo na mtu yeyote mbali hata na wale pale” – Roma Mkatoliki
Hii ndio status ya Roma Mkatoliki dec 13 2012.

MAGAZETI YA LEO JAN 7 NDIO HAYA NA STORI KUBWA ZA MICHEZO NA HARDNEWS.

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.