Wednesday, July 3, 2013

ASKOFU WA JIMBO KATOLIKI LA IRINGA ATOA DARAJA LA UPADRE KANING’OMBE




                                                                Kanisa la Parokia ya Kaning'ombe
Askofu Mkuu wa Jimbo la Iringa Tarcisius Ngalalekumtwa
                                                              Baba Askofu akielekea altare

                                       Shemasi Victorino Kalinga Aliyepata daraja la Upadre
Baba Askofu akiwa Tayari kumtunuku daraja la upadre Shemasi Victorino Kalinga

 Hapa anapewa upadre
Hapa Tayari ametunukiwa daraja la Upadre



 Mmiliki wa mtandao huu ndugu Lewis Mbonde katikati mwenye koti nyekundu akiwa kazini na Thobias Myovela wa Radio Maria kushoto na Gustav Chahe Kulia aliyesimama mmiliki wa Gustav Chahe blog

Na Gustav Chahe,Lewis Mbonde na Thobias Myovela Iringa
RAIS wa Baraza la Maaskofu Tanzani Mhashamu Tarcisius Ngalalekumtwa amewataka watu wasiwe wasanii kwa kutumia jina la Mwalimu Nyerere kuwa wanamuenzi huku wakifanya mambo ya ajabu ya unyanyasaji na ukandamizaji wa haki za watu.
Aliyasema hayo katika maadhimisho ya Misa utoaji wa daraja la Upadre kwa Shemasi Victorino Kalinga iliyokwenda sambamba na maadhimisho ya Yubilei ya Miaka 75 ya Parokia ya Kaning’ombe jimbo Katoliki la Iringa.
Askofu Ngalalekumtwa ambaye pia ni askofu wa Jimbo Katoliki la Iringa alisema, kutokana na usanii wa watu wanaojifanya wanamuenzi hayati Baba wa Taifa Julius Nyerere huku wakifanya mambo ya kihuni ipo siku uongo wao utawatokea puani.
“Ipo siku mtasema mnamuenzi halafu mmkute ameketi juu ya kaburi sijui mtasema nini? Nyie watu wadanganyifu mnaotumia jina la Mwalimu Nyerere, acheni usanii, uhuni na uongo kuwadanganya watu wenye akili” alisema.
Alisema kuwa si kila mtu amefirisika kifikra na kwamba watu wanajua kila kitu kinachoendele kuwa ni uongo au ukweli.
Alisema binadamu wa leo ametoka nje ya matakwa ya Mungu na kufanya mambo yasiyo stahili kwa kutenda dhambi kwa kujifanya wema huku wakiwaumiza wenzao.
Aliwaasa Wakristo kuwa wajumbe wa habari njema kwa ajili ya kulinda amani ambapo wanatakiwa kumtafuta Mungu kwa ajili ya wokovu.
“Maaskofu na Mapadre wameteuliwa na Mungu kwa ajili ya kufungua mioyo ya watu ili waweze kumtafuta Mungu na kuufifikia wokovu wa wa milele.
“Mungu mwenye upendo, huruma na msamaha ni Yule tunayehitaji kuajikabidhi maisha yetu kwa ajili ya furaha ya milele” alisema askofu Ngalalekumtwa.
Hata hivyo alisema Padre anapasika kuwa na msimamo usio na lawama ili asije akachakachua maagizo ya Mungu na kujitunza nafsi yake kwa ajili ya kuwa muangalizi mwema wa kondoo alioachiwa na Mungu.
“Padre awe na msimamo safi na awe na akili kichwani ili apate kubaini kufichua na kukemea yale ambayo hayastahili yanyowafanya wana wa Mungu kuishi kwa hofu. Padre ni mjumbe wa amani ambaye anatakiwa kuwa mstari wa mbele kwa ajili ya kuishi kwa upendo, mshikamano na kuwahurumia wengine” alisema.
Alisema kuwa pamoja na purukushani zote zilizopo, bianadamu ana kiu ya Mungu ambayo padre anatakiwa kuizima kiu hiyo.
Alisema kuwa wakristo wanatakiwa kukusanyika pamoja na kutoa dua kwa Mungu ili kuliombea Taifa linaloingiliwa na watu wasio na mapenzi mema wanaopenda kuwasambaratisha watu wasio kuwa na hatia.
Miaka 75 ni heshima tuliyopewa na Mungu kwa ajili ya kutangaza uweza wake kwa mataifa ambayo bado hayajamfahamu.
“Miaka 75 iwe ishara ya kuendeleza na utamaduni wetu wa upendo aliotuachia Kristo Mwokozi kwa ajili ya maisha yetu. Lindeni hayo ili Mungu Mwenyezi azidi kutulinda katika ukamilifu wa upendo, mshikamano, huruma, hekima, busara na amani” alisema.
Kanisa lazima litoe lishe kwa watu wake ili miili yao isishambuliwe na magonjwa ya dhambi. Kwa njia ya padre, binadamu watapata faraja ya Mungu kwetu tunaoishi katika bonde la machozi.
Maadhimisho ya upadre yalikwenda sambamba na maadhimisho ya Yubilei ya miaka 75 ya Parokia ya Kaning’ombe ambapo yalihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kiroho na serikali ndani na nje ya jimbo hilo.

MADEE AMPONGEZA DOGO JANJA


Na Elizabeth John

KIONGOZI wa Kundi la Tip Top Connection, lenye maskani yake Manzese jijini Dar es Salaam, Ahmed Ally ‘Madee’, amesema amevutiwa na kazi ya msanii nyota katika muziki wa kizazi kipya nchini, Abdulazizi Chende ‘Dogo Janja’ inayoendelea kufanya vyema katioka vituo mbalimbali vya radio.

Kauli hiyo imekuja baada ya wapenzi wa muziki huo, kufikiria kwamba Madee angeichukia ngoma hiyo ya Dogo Janja inayokwenda kwa jina la  ‘Ya Moyoni’ kwa kuhisi kuwa imemzungumzia yeye lakini haijawa hivyo.

Akizungumza Dar es Salaam, Madee alisema kuwa bado ni shabiki mkubwa wa Dogo Janja na anampongeza sana kwa kufanya vizuri na ngoma hiyo inayoendelea kufanya vyema katika vituo mbalimbali vya radio.

Madee alisema amependa zaidi kiitikio kilichofanywa na PNC lakini ameongeza kuwa kama angeisikia kabla ya kupelekwa redioni angependekeza yafanyike marekebisho kadhaa.

Miezi kadhaa iliyopita Madee na Dogo Janja walikuwa gumzo kwenye vyombo vya habari vya Tanzania baada ya Madee kushutumiwa kumtumia msanii huyo isivyotakiwa kiasi cha kufanya aondoke katika kundi hilo.

WACHINA WAKABIDHI UWANJA WA TAIFA LEO


 Balozi wa China, Lu Youqung akiweka sahihi katika hati ya makabidhiano ya uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, leo. Kulia ni Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara.
  Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Sihaba Nkinga na Balozi wa China, Lu Youqung wakati wa hafla ya makabidhiano ya uwanja wa Taifa.
Balozi wa China, Lu Youqung  akimkabidhi ufunguo Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Fenella Mukangara kama ishara ya makabidhiano rasmi ya uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, leo.


Monday, July 1, 2013

KIJANA AFANYA MAAJABU ATEMBEA HEWANI



British Magician called Dynamo was spotted flying in the air whiles holding a moving bus. Magician Dynamo ‘catches a ride’ on a London bus leaving tourists and Londoners spellbound. The 30-year-old appeared to hover beside the double decker as it visited several of the city’s landmarks.
Although it was clear something was up on the number 543 bus (which does not exist in real life),  anybody who saw the stunt couldn’t understand how he had actually pulled it off.
The illusionist, whose real name is Steven Frayne, was promoting Pepsi Max’s Live for NOW campaign, but is is not the first time he has taken the public’s breath away.


SEHEMU YA UJIO WA OBAMA ITAKAVYO KUWA KATIKA ANGA YA TANZANIA NA DAR ES SALAAM ITAKUWA HIVYO



Ndege maalum ya kivita itasindikiza Air Force One ya Rais Bar
ack ObamaWalinzi wa rais Obama kama wanavyoonekana

MSAFARA wa Ndege ya Rais wa Marekani Barack Obama, yawezekana ndiyo msafara uliowai kupata ulinzi mkali kuliko zote.
Air Force One ambayo ndiyo ndege inayotumiwa na marais wote wa marekani,ndege hii ulindwa kwa asilimia mia moja.

Hata hivyo ulinzi wa ndege hii wakati wa utawala wa Rais Obama imekuwa tofauti baada ya kuongezewa ulinzi kuliko hata ilivyokuwa kwa mtangulizi wake George Bush.

Wakati wa Bush ndege hii ilikuwa inalindwa na ndege za kivita 10 lakini katika utawala wa Obama ndege hii inalindwa na ndege za kivita 15,wakati wote ikiwa angani.

AIR Force One hutembea katikati ya ndege sita za kijeshi,juu ya ndege ya Rais huwa kuna ndege mbili za kivita,chini ya ndege hiyo kuna ndege mbili, mbele ya ndege hiyo kuna ndege moja na nyuma kuna ndege moja.

Umbali wa kilomita 300 baada ya ndege ya Rais Obama kupita kuna kuwa na ndege mbili za kivita zenye mwendo kasi, kabla ya ndege ya Rais kupita kuna kuwa na ndege tisa zinazokwenda kwa mwendo kasi na sambamba kwa umbali wa kilomita zaidi ya 500.

SOMA MAGAZETI YA JUMATATU 01/07/2013


Magazeti ya Jumatatu 01/07/2013 na yaliyochomoza na Mapokezi ya Obama Dar


DSC 0232 761c6
DSC 0233 b4230
DSC 0234 1d864
DSC 0235 9e17a
DSC 0236 6e64b
DSC 0237 94547
DSC 0238 2e7ef
DSC 0239 05ce5
DSC 0240 972ae
DSC 0241 df438
DSC 0242 46db0
DSC 0243 48ae2
DSC 0244 56b97
DSC 0245 b5440
DSC 0246 d580b

RAIS WA ZAMANI WA CHAD AKAMATWA NCHINI SENEGAL


http://images.lpcdn.ca/641x427/201306/30/710670-ex-president-tchadien-hissene-habre.jpgRais wa zamani wa Chad, Hissene Habrehttp://www.senenews.com/wp-content/uploads/2012/11/hissenehabre.gif 
Rais wa zamani wa Chad, Hissene Habre akitafakari jambo.
 
POLISI nchini Senegal , wamemkamata rais wa zamani wa Chad, Hissene Habre, aliyekuwa anatafutwa kwa madai ya ukiukwaji wa haki za binadamu wakati wa utawala wake wa miaka 8.
Wakili wa Bwana Habre, El Hadji Diouf, alisema kuwa alikamatwa na polisi kutoka nyumbani kwake mjini Dakar na kupelekwa sehemu isiyojulikana.

Habre mwenye umri wa miaka 70, amekuwa akitumikia kifungo cha nyumbani, nchini Senegal tangu mwaka 2005 alikokimb
ilia baada ya kung'olewa mamlakani mwaka 1990.

Aanatuhumiwa kuwatesa maelfu ya watu, wanaominika kuwa wapinzani wake.

Mwaka jana mahakama ya kimataifa ya haki, iliamuru Seengal kumchukuliwa hatua za kisheria au kupeleka kwingineko ambako atakabiliwa na sheria kwa uhalifu aliotenda.

Kukamatwa kwake kunakuja siku kadhaa baada ya rais wa Marekani, Barack Obama kumsifu rais Macky Sall kwa hatua zake za kuelekea katika kumfungulia mashtaka Habre mwanzoni mwa ziara yake ya Afrika.

Mashirika ya kutetea haki za binadamu, yamekuwa yakishinikiza Senegal kwa miaka mingi, kumfungulia mashtaka Habre.

Tuhuma anazokabiliwa nazo ni za tangu mwaka 1982, wakati alipoingia mamlakani hadi mwaka 1990 alipoondolewa uongozini kwa njia ya mageuzi.

Habre alishtakiwa kwa mara ya kwanza nchini Senegal mwaka 2000, lakini mahakama za nchi hiyo ikaamua kuwa wakati huo isingeweza kushtakiwa huko.

Waathiriwa wa utawala wake baadaye waliwasilisha malalamishi chini ya sheria ya kimataifa ya Ubelgiji ambayo inaruhusu majaji wake kusikiliza na kuhukumu washukiwa wa kesi za ukiukwaji wa haki za binadamu kokote duniani.

Hata hivyo Senegal imekataa ombi la Ubelgiji kumhamisha nchini humo ili ahukumiwe. BBC

MASANJA, SHILOLE WAFIKA ULIPO MJENGO WA UBALOZI WA TANZANIA MAREKANI


 Juu na chini ni Wasanii Masanja Mkandamizaji na Shilole wakiwa nje ya mjengo wa Ubalozi wa Tanzania, Washington, DC mara walipopita na kupiga picha nje ya mjengo Jumapili June 30, 2013 walipokua wakitokea uwanja wandege wa kimataifa wa Dulles uliopo Sterling, Virginia. Kesho mchana Jumanne April 2, 2013 watatembelea rasmi mjengo huo na kusaini kitabu cha wageni.
 Masanja na Shilole wakiwa na mwenyekiti wa kamati ya maandalizi wakiangalia menyu tayari kwa kuagiza dinner ya mchana walipokwenda mgahawa wa kijiji cha Swahili uliopo Beltsville, Maryland
 Shilole na Masanja katika picha ya pamoja na mmiliki wa mgahawa wa Swahili Village Bwn.Kelvin.
Masanja na Shilole wakiingia kwenye usafiri wao kuelekea Hotelini walikofikia.

OBAMA ATUA DAR ES SALAAM, SHUGULI ZA KUONGOZA NDEGE ZAFANYWA NA WAMAREKANI WENYEYE



 Helikopta ya Polisi ikiwa katika doria ya hapa na pale, hata hivyo eneo lote la uwanja wa Ndege ulidhibitiwa na Wamarekani wenyewe ikiwemo na kazi ya kuongoza ndege.  (Picha na Habari Mseto Blog)
Ulinzi kila kona
 Rais Barack Obama wa Marekani akiwa na mwenyeji wake Rais Jakaya Kikwete mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. (Picha na Habari Mseto Blog)
 Rais Barack Obama wa Marekani akiwa na mwenyeji wake Rais Jakaya Kikwete mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Rais Barack Obama wa Marekani akiwa na mwenyeji wake Rais Jakaya Kikwete mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Rais Barack Obama wa Marekani akikagua gwaride la heshima wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo.
 Rais Baracka Obama akiwapungia wakiangalia vikundi vya ngoma.
 Ulinzi ulimarishwa.
 Bendera ya Tanzania ikiwekwa katika gari lililombeba Rais wa Marekani, Barack Obama.
Gari alilopanda Rais Obama
 Rais Barack Obama akishuka katika ndege iliyomleta huku akifuatana na familia yake.
Rais Obama na mkewe wakipokea maua.