Friday, May 3, 2013

PICHA ZA POLISI ALIEPIGWA RISASI NJE YA UKUMBI ALIPOKUA ANAAPISHWA WAZIRI WA KWANZA MWEUSI NCHINI ITALIA

.
.
Ripota wa nguvu Michael Minja kutoka nchini Italia, anaripoti kwamba baada ya kuchaguliwa kwa mara ya kwanza kwa Waziri mwenye asili ya Kiafrika kwenye historia ya Italia ambae ni CECILE KYENGE KASHETU kutokea Congo DRC, alijitokeza mwanaume mmoja na kuwapiga risasi polisi wawili waliokuwemo nje ya Ukumbi walikokua wanaapishwa Mawaziri wapya Ikulu.

Mtu mmoja alijotokeza na kuwashambulia Polisi kwa kuwapiga Risasi wakati wakiwa wanaendeleza ulinzi katika eneo hilo ambapo Polisi mmoja alijeruhiwa vibaya kwa risasi shingoni lakini hakupoteza maisha.
Mtuhumiwa anashikiliwa na Polisi ambapo habari zisizo rasmi zimeeleza kwamba kuna uwezekano alikua na matatizo ya akili au uamuzi huo unahusika na ubaguzi wa rangi baada ya kuteuliwa kwa Waziri mpya wa mambo ya nje ambae ni Mweusi.
.
.
.
.
.
Huyu ndio Waziri wa kwanza mweusi kwenye historia ya Italia, aliolewa na Muitaliano miaka mingi iliyopita na kuhamia pamoja na kuchukua uraia wa Italia mwaka 1983.

KUHUSU RAIS WA BOTSWANA KUJERUHIWA NA MNYAMA DUMA.

.
.
Serikali ya Botswana imesema Rais wa nchi hiyo Ian Khama ameshonwa nyuzi baada ya kung’atwa na mnyama aina ya duma aliekua analishwa kwenye sehemu anakohifadhiwa.
Ilikua kwenye kambi ya jeshi pale ambapo mnyama huyo alimrukia Rais Ian aliekua na walinzi wake.
Pamoja na kwamba Rais Ian baadae alionekana amewekewa plasta kwenye majeraha, msemaji wa Serikali amesema majeraha aliyoyapata ni madogo sana.
Duma ambao ni Wanyama wenye kasi kubwa zaidi ardhini ni moja ya Wanyama waliopo kwenye tishio la kutoweka Afrika, wamebaki elfu 12 na 400 tu kwenye baadhi ya nchi ikiwemo Botswana.
.
tukio jingine.
Ripoti kutoka kusini kwa Kentucky Marekani zimetaarifu kwamba mtoto wa miaka miwili ameuwawa kwa risasi na kaka yake mwenye umri wa miaka mitano aliekua anachezea bunduki aliyokua amezawadiwa.
Hiyo bunduki ilikua kwenye kona ambayo wazazi waliisahau pia kuitoa risasi ndani yake….. mtoto huyo wa kiume akaichukua na kuanza kuichezea wakati huo mama alikuepo nyumbani lakini hakuwa amemuona.
Kwa bahati mbaya akafyatua risasi ambayo moja kwa moja ilimlenga mdogo wake mwenye umri wa miaka miwili ambae ni alikimbizwa hospitali na baadae kufariki…. pamoja na uzito wa tukio huyu mtoto aliefariki atafanyiwa uchunguzi kwenye mwili kama risasi alipigwa kwa bahati mbaya ama ilikua ni kitu kingine.
.
.
.

MAGAZETI YA MAY 3 2013 KWENYE KURASA ZA MWANZO NA MWISHO

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

.
.
.

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

MAGAZETI YA MAY 2 2013

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

.
.
.
.
.
.
.
.