Thursday, January 3, 2013

PICHA 15 ZA MSIBANI HAPA NYUMBANI ALIPOKUA AKIISHI SAJUKI.

Hii ndio nyumba aliyokua akiishi mwigizaji Sajuki Tabata Dar es salaam.
.
.
Huyo wa katikati ndio mama mzazi wa Sajuki.
.
Millard Ayo na Mwigizaji Dinno mmoja kati ya marafiki wa karibu sana wa Sajuki.
Huyu ni baba mzazi wa Sajuki ambapo alitoka Songea kuja kumuuguza mwanae.
.
.
.
.
.
Baadhi ya waigizaji wa bongo movie.
.

HABARI KUBWA ZA KURASA ZA MWANZO NA ZA MWISHO MAGAZETINI LEO..


.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

Watu 20 wafariki kwenye ajali Kenya

Matatu iliyohusika kwenye ajali hiyo
Takriban watu ishirini wamefariki kwenye ajali mbaya ya barabarani nchini Kenya, baada ya gari moja ya abiria maarufu kama matatu, kukosa mwelekeo na kutumbukia ndani ya chimbo la mawe.
Ripoti zinasema watu wengine saba wako katika hali mahututi.
Gari hilo ambalo linaruhusiwa kubeba abiria kumi na wanne pekee inasemekana kubeba zaidi ya abiria 28.
Ajali hiyo ilitokea magharibi mwa nchi hiyo ambako barabara ni mbovu na inatokea siku moja tu baada ya watu wengine kumi na moja kufariki katika eneo hilo hilo.
Idara ya polisi nchini humo imeanzisha uchunguzi kufuatia ajali hiyo.
Afisa mkuu wa polisi katika eneo hilo amesema, maafisa wa polisi watachukuliwa hatua za kisheria ikiwa itabainika kuwa gari hilo lilipita katika kituo chochote cha ukaguzi na hakiku kamatwa kwa kubeba abiria kupita kiasi.

Kesi dhidi ya Cecil yafutiliwa mbali Uganda

 
David Cecil akiwa korokoroni
Mahakama moja nchini Uganda, imefutilia mbali kesi dhidi ya mwandishi mmoja wa michezo ya tamthilia, David Cecil, ambaye alikuwa akikabiliwa na shtaka la kuonyesha mchezo kuhusu hali ya wapenzi wa jinsia moja, katika mji mkuu wa nchi hiyo Kampala.
Bwana Cecil, alikabiliwa na tuhuma za kukiuka sheria kwa makusudi.
Bwana Cecil ameiambia BBC, kuwa kesi hiyo ilifutiliwa mbali kutokana na kile alichokitaja kama ukosefu wa ushahidi wa kutosha dhidi yake.
Mshukiwa huyo alikamatwa mwezi Septemba, kwa kukiuka sheria za hiyo kwa kuonyesha mchezo huo bila kibali wenye maudhui ''The River and the Mountain''

Mapenzi ya jinsia moja imeharamishwa nchini Uganda.

Bunge la nchi hiyo linajadili uwezekano kwa kuimarisha adhabu ya wale watakaopatikana wakijihusisha na mapenzi ya jinsia moja.
Rais wa Uganda akikagua gwaride la kijeshi
Ikiwa angelipatikana na hatia Bwana Cecil, angelihukumiwa kifungo cha miaka miwili gerezani.
Alipigwa faini ya laki tano pesa za Uganda, sawa na dola mia mbili za Marekani.
Akiongea muda mfupi baada ya kesi dhidi yake kufutiliwa mbali Bwana Cecil alisema kuwa amefurahishwa na uamuzi huo, licha ya hofu kuwa huenda akafunguliwa mashtaka mengine.
Wakati huo huo, Wabunge wa Uganda, wanajaribu kuitisha Bunge likatishe kipindi cha mapumziko ili lijadili kukamatwa kwa baadhi ya wabunge kuhusiana na kifo cha mbunge mwanamke wa wilaya ya Butaleja, mashariki mwa Uganda, wiki mbili zilizopita.
Kifo hicho kimezusha hofu na mabishano ya kikatiba baina ya Rais Yoweri Museveni na wabunge.
Ili kufanikisha ombi hilo, inapasa kwa uchache wabunge 125 walitie sahihi na kisha kulifikisha kwa Spika, mwenye uwezo wa kulirudisha Bunge.

Wanajeshi wa kigeni watumwa Afrika ya Kati

 
Wanajeshi wa waasi katika Jamuhuri ya Afrika ya Kati
Jeshi la eneo la Afrika FOMAC katika Jamhuri ya ya Afrika ya kati kwa sasa linaimarishwa na vikosi vya mataifa jirani wakijumuisha wanajeshi elfu mia moja na ishirini kutoka Jamuhuri ya Demokrasi ya Congo DRC.
Kamanda wa FOMAC, amesema kuwa wanjeshi hao wataenda kuulinda mji wa Damara, dhidi ya waasi wanokaribia jiji kuu la Bangii.
Ripoti zinasema wanajeshi hao wa waasi wafika takriban kilomita sabini na tano hivi kutoka mji mkuu wa Bangui.
Msemaji wa waasi hao jijini Paris, anasema ameliambia shirika la Reuters kuwa wamesitisha kidogo safari yao na huenda wakajianda kwa mazungumzo ili kupata suluhu ya kisiasa.
Serikali ya Gabon imesema kuwa itatuma kikosi cha wanajeshi 120, huku serikali ya Cameroon vile vile ikitarajiwa kutuma kiasi kama hicho
Hili ndilo tishio kubwa zaidi kuwahi kukumba serikali ya rais Francois Bozize, tangu alipotwaa uongozi wa taifa hilo kupitia mapinduzi ya serikali mwaka wa 2003.
Waasi wao wa Seleka, walianza kampeini dhidi ya serikali ya mwezi uliopita na tarayi wameteka miji kadhaa ikiwemo mji wa Bria ulio na utajiri mkubwa wa madini la Almasi.