Saturday, December 1, 2012

Chris Brown na Rihanna.
Wiki moja baada ya mwimbaji Rihanna kupost kwenye page yake ya mtandao wa Instagram picha ya Chris Brown akiwa kitandani bila shati, time hii Rihanna amezidi kuvipa vyombo vya habari cha kuongea baada ya kupost picha nyingine.
Picha yenyewe ni hiyo hapo kushoto ambapo sasa inazidi kujulikana kabisa kwamba Rihanna na Chris Brown ambao ni wapenzi wa zamani wamerudiana japo hawajawahi kutamka.
Kwa mujibu wa Necole, baada ya kuiweka hii picha RiRi aliandika “I don’t wanna leave! Killed it tonight baby”
Kwenye moja ya interview zake mwaka huu, Rihanna alisema bado moyo wake unamkubali sana Chris Brown na ni ngumu kumsahau maishani.
Picha hizi za Instagram zimezagaa siku kadhaa tu baada ya Chris Brown kutangaza kwamba ameachana na mpenzi wake ili kurejesha amani manake hakua anapenda akiona urafiki wa Chris na Rihanna unaendelea.
.
Baada ya marafiki wa karibu kuthibitisha kwamba siku za mwisho Marehemu Sharo Milionea aliwahi kukiri kwamba anahisi amelogwa na alikua hana amani, mama yake mzazi leo amezungumza na Amplifaya.
Baada ya kuwasikia  waigizaji Kitale na Mzee Majuto wakisema ni kweli Sharo Milionea alikiri kwamba anahisi amelogwa watu wengi walikua na kiu ya kufahamu kama Sharo aliwahi kumwambia mama yake.
.
Akiongea kwenye Exclusive interview na AMPIFAYA ya CLOUDS FM kijijini kwao Muheza Tanga, mama mzazi wa Sharo mwenye umri wa miaka 52 amesema Sharo hakuwahi kumwambia chochote kuhusu kulogwa au kutokua na amani maishani mwake.
Namkariri akisema “sijawahi kusikia chochote hata siku moja na wala sihisi chochote naona ni mipango ya Mungu tu, marafiki zake ndio walionielezea kwamba Sharo alikwenda kwa rafiki yake akawa kama mtu mwenye wasiwasi akasema najisikia vibaya toka nilipotoka kwangu lakini nilipofika kwako najisikia nimepona, baada ya hapo ndio akaondoka kwenda Tanga”
Mama mzazi wa Sharo Milionea ambae jana alisema hakuwa na taarifa kama Sharo Milionea alikua anakuja Tanga siku alipopata ajali ikiwa ni kawaida yake kutokutoa taarifa, amesema Sharo Milionea alikua tayari amenunua kiwanja Mbezi Dar es salaam na siku za mwisho alimtamkia kwamba anataka kuoa manake amechoka kuishi peke yake.
Hawa ni mashabiki wa timu ya Gormahia ya Kenya ambao waliangua vilio baada ya timu yao kushindwa.
.
Hizi picha za Wakenya nilizozipata zinanikumbusha yule shabiki wa Yanga kwenye hiyo video hapo chini ambae aliangua kilio uwanjanibaada ya kuona timu yake imehujumiwa.

MASTAA WA AFRICA NILIOKUTANA NAO 2012.

Posted: 1st December 2012 by MillardAyo in News
1
Hizi picha zote ni wakati nikiwa Johannesburg South Africa kwa ajili ya kuhudhuria tuzo za Channel O.
.
Wyre kutoka Kenya.
Keko kutoka Uganda.
.
Tiwa Savage kutoka Nigeria.
Camp Mulla kutoka Kenya.

.
Dj Cleo kutoka South Africa.
Ice Prince kutoka Nigeria.
Toya Delazy kutoka Afrika kusini.
Ukumbi palipofanyika tuzo za Channel O 2012, ulitengenezwa Soweto maalum tu kwa ajili ya tuzo baada ya hapo unabomolewa.
.
Ay
.
.
Donald Mr i deserve kutoka Afrika Kusini.

PICHA ZA KWANZA ZA UHURU SULEIMAN MAZOEZINI AZAM FC.

Posted: 30th November 2012 by MillardAyo in News
0
Mchezaji wa zamani wa Simba Sc Uhuru Suleiman akiwa na jezi ya Azam FC kwenye mazoezi kwenye uwanja wa Chamazi Complex unaomilikiwa na club hiyo aliyohamia.
.
Kwenye picha ya kwanza ni Mshambuliaji wa timu ya Kenya Anthony Kimani akimiliki mpira mbele ya beki wa timu ya Ethiopia, Abdulkarim Hassen Yigemo wakati wa mchezo wa Cecafa Challenge uliochezwa katika Uwanja wa Nelson Mandela Jijini Kampalaambapo Kenya imeshinda 3-1 na kuingia robo fainali.
Shabiki wa Kenya. (shaffihdauda.com ndio mwandishi )
0

Warembo wakisubiri kuchujwa ili waingia kwenye video shooting.
.
.
.
.
Hawa ni ambao wameshapita tayari.
.
.
.
Hawa wengi wao hawakufaulu kwenye mchujo.
.
.
.
.
.

.
.
.
Ay na Fa walikua pamoja, Fa ameuza pia ndani ya video.



.
.
.
.

.
.
.

.

.


Polisi wamwaga tena damu ya raia

  *Yu mahututi wodini Muhimbili
  *Vurugu zatanda, barabara yafungwa
Askari Polisi wakilinda doria eneo la Tegeta kwa Ndevu baada ya kutokea vurugu ambapo mtu mmoja alidaiwa kujeruhiwa na pilisi Jijini Dar es Salaam jana na kukimbizwa hospitali kwa matibabu.
Vurugu kubwa zilizohusisha ufyatuaji wa mabomu ya machozi na risasi za moto kati ya askari wa Jeshi la Polisi na wananchi, jana zilizuka katika eneo la Tegeta, jijini Dar es Salaam na kusababisha kijana anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 17 kujeruhiwa kwa risasi kichwani.

Kijana huyo amefahamika kwa jina la John Massawe, ambaye alikumbwa na mkasa huo alipokuwa dukani akiuza magodoro.

Vurugu hizo zilizuka majira ya saa 4:45 asubuhi katika eneo maarufu kama “Tegeta kwa Ndevu”.

Habari kutoka eneo hilo zinaeleza kuwa vurugu hizo zilizodumu kwa takriban dakika 15, zilisababishwa na baadhi ya maofisa wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads).

Maofisa hao wa Tanroads wanadaiwa kufika katika eneo hilo wakiwa na magari ya kunyanyua na kuvuta vitu vizito, maarufu kama “Break Down” na kutaka kuyakamata magari yaliyokuwa yameegeshwa pembezoni mwa barabara.

Kwa mujibu wa habari hizo, baada ya kufika katika eneo hilo, maofisa hao wa Tanroads walianza kuyakamata magari hayo.

Kitendo hicho kilipingwa na wananchi, ambao walianza kuwazuia maofisa hao wa Tanroads, huku wakiwazonga.

Hali hiyo ilisababisha askari polisi kuitwa, ambao baada ya kufika, waliwaamuru wananchi kutawanyika, lakini amri hiyo ikapuuzwa.

Kutokana na amri hiyo kupuuzwa, askari hao walianza kufyatua risasi hewani pamoja na mabomu ya machozi na kuzua tafrani na hofu kubwa katika eneo hilo.

Katika tafrani hiyo, mmoja wa askari polisi anadaiwa kumpiga mtoto huyo risasi kichwani na kudondoka hapo hapo.

Milio ya risasi za moto iliendelea kurindima katika eneo hilo, huku mtoto huyo akiwa amelala chini akitokwa damu nyingi bila ya msaada wowote.

Kutokana na hali hiyo, wananchi hao walianza kukimbia hovyo, huku wafanyabiashara wa maduka yaliyopo karibu na tukio zilipotokea vurugu hizo wakilazimika kuyafunga.

Baada ya dakika 15 kupita, hali ilirejea kuwa ya kawaida na wananchi walianza kujikusanya makundi makundi wakijadili mkasa huo.

Majira ya saa 7:52 mchana wananchi hao waliamua kufunga barabara kwa kutumia magogo, madaraja ya mbao na matenga.

Hatua hiyo ilisababisha magari kushindwa kuendelea na safari zake na hivyo kusababisha msongamano mkubwa wa magari kwa muda katika eneo hilo.

Dakika chache baadaye, Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Wazo, Mponjoli Mponjoli, akiwa ndani ya gari la polisi lenye namba PT 2083, alifika katika eneo hilo.

Baada ya kufika, alishuka kwenye gari lake na kuanza kuwasihi wananchi hao kuacha vurugu na kuwataka wawe na subira.

Pia lilifika gari lingine la polisi aina ya Land Cruiser lenye namba za usajili MX 54 UKH, likiwa na askari, ambao walishuka na kuanza kuondoa vizuizi.

Hata hivyo, licha ya Mponjoli kuwasihi hivyo, wananchi hao walipuuza na kuanza kuimba nyimbo za kutaka haki itendeke.

Sanjari na kuimba nyimbo hizo, wananchi hao waligoma kuondoka kwa madai ya kutaka hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya wahusika waliosababisha vurugu hizo.

Hali hiyo ilionekana kumzidi Mponjoli na hivyo, iliilazimu makao makuu ya jeshi hilo kuongeza nguvu kwa kumtuma  Mkuu wa Operesheni maalum wa Jeshi la Polisi nchini, Simon Sirro, ambaye alifika eneo hilo na kuwasihi wananchi hao kuwa watulivu na kuwaahidi kuwa upelelezi wa tukio hilo utafanyika.

Hata hivyo, wananchi walioonekana kuwa na jazba, walisema wanaostahili kulaumiwa ni Tanroads kwa kushindwa kuweka vibao katika sehemu zisizoruhusiwa kuegesha magari.

“Hii inaonekana kama biashara. Yaani hawa watu wanapokuta gari lako bila kuuliza wanaita ‘break down’ na kulifunga. Ukilipa pesa wanayotaka wanakuachia. Kwanini hawaweki vibao vya kuonyesha kuwa sehemu fulani haziruhusiwi kupaki magari?” alihoji mwananchi aliyejitambulisha kwa jina la Boniface Masumbuko.

Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.

Alisema tukio hilo lilitokea baada ya Kampuni ya Udalali ya Mwakinga kukamata gari lililokuwa limeegeshwa sehemu hiyo ambayo hairuhusiwi kuegesha magari.

Kamanda Kenyela alisema baada ya kukamata gari hilo, wananchi walianza kuwarushia mawe na kusababisha askari polisi kufika kwa ajili ya kutoa msaada.

Alisema hata baada ya polisi kufika, wananchi waliendelea na vurugu za kurusha mawe na katika vurugu hizo kuna mtu alijeruhiwa.

Hata hivyo, alisema taarifa za kuwa kuna mtu aliyekufa katika vurugu hizo si za kweli, bali alijeruhiwa na kukimbizwa katika Hospitali ya Mwananyamala, ambako anaendelea na matibabu.

HOSPITALI YA MWANANYAMALA WAZUNGUMZA

Katibu wa Afya wa Hospitali ya Mwananyamala, Edwin Bisakala, alithibitisha kuwapo kwa majeruhi huyo hospitalini hapo.

Alisema walimpokea kijana huyo majira ya saa 6:00 mchana na kumpatia huduma ya kwanza.

Bisakala alisema, mtu huyo alipata majeraha makubwa kichwani na walimpatia huduma ya kwanza na kumpeleka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH)  kwa matibabu zaidi.

“Ni kweli tumempokea majeruhi wa aina hiyo. Tulimtibu na kumpeleka Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu. Kwa kuwa alikuwa anahitaji matibabu zaidi,” alisema Bisakala.

HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI WAZUNGUMZA

Afisa Habari wa MNH, Aminieli Eligaesha, aliliambia NIPASHE jana jioni kuwa walimpokea mgonjwa huyo kutoka Hospitali ya Mwanayamala majira ya mchana akiwa katika hali mbaya na kupelekwa katika Chumba cha Wagonjwa Mahututi (ICU) hospitalini hapo.

Alisema hadi jana hali yake ilikuwa mbaya na madaktari walikuwa wanaendelea kumpatia matibabu zaidi.
CHANZO: NIPASHE

HIVI NDIVYO MWANAHABARI DAUD MWANGOSI ALIVYOPOTEZA MAISHA LEO KTK VURUGU ZA CHADEMA NA POLISI



Hapa polisi wakiwataka wafuasi wa Chadema kutawanyika eneo la tukio ofisi za Chadema Nyololo Mufindi

Mwili wa mwanahabari Daud Mwangosi ukiwa chini


Daud Mwangosi kulia enzi za uhai dakika 20 kabla ya kuuwawa kwake
Mwandishi wa habari wa Chanel Ten mkoa wa Iringa na Mwenyekiti wa chaa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Iringa Daud Mwangosi ameuwawa katika vurugu za Polisui i na wafuasi wa Chadema katika kijiji cha Nyololo wilaya ya Mufindi mkoani Iringa leo

Mwanahabari huyo Daud Mwangosi aliuwawa majira ya saa 10 jioni katika ofisi za Chadema Nyololo huku askari mmoja akijeruhiwa vibaya kwa risasi .

Kabla ya kuuwawa kwa mwanahabari huyo mabomu yaliweza kupigwa eneo hilo kuwatawanya wafuasi hao wa Chadema ambao walikuwa wakigoma kutawanyika eneo hilo na kuamua kukaa chini kuwa haapo tayari kuondoka katika ofisi yao.

Chanzo cha mwanahabari Mwangosi kuuwawa klitokana na kukamatwa kwa mwandishi wa habari wa gazeti la Nipashe mkoa wa Iringa Godfrey Mushi na hivyo mwanahabari huyo kkutaka kuhoji polisi sababu ya kukamatwa kwa mwanahabari huyo ndipo askari hao walipoanza kumshambulia kwa kichapo na baadae mlio kama wa bomu ulisikika eneo hilo na mwandishi huyo na askari mmoja waliaguka chini .

Ndani ya dakika tano ilisikika sauti kutoka kwa askari huyo kuwa afande nimekufa ndipo walipomchukua na kumpeleka Hospitali ya wilaya ya Mufindi huku mwili wa mwanahabari huyo ukipelekwa chumba cha kuhifadhia maiti .

Katika vurugu hizo zilizodumu kwa takribani dakika 30 kwa askari na wafuasi wa Chadema kurushiana mawe kwa mabomu zaidi ya magari matano ya Chadema na ya wananchi yameharibiwa huku watu kadhaa wamejeruhiwa na mwanahabari mmoja Godfrey Mushi akijeruhiwa vibaya.

Hii ni taarifa ya Jeshi la polisi kabla ya tukio kwa vyombo vya habari


JESHI la polisi mkoa wa Iringa limesema limezuia mikutano ya vyama vya siasa kwa vyama vyote na sio kwa chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) pekee hivyo laonya vyama vyote kutii sheria bila shuruti.

Hata hivyo jeshi hilo la Polisi limesema kuwa halifanyi kazi kwa matakwa ya chama chochote cha siasa na kuwa si kweli kama wanavyodai viongozi wa Chadema kuwa jeshi la polisi linatumiwa na chama cha mapinduzi (CCM) kuzuia mikutano hiyo.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Michael Kamuanda ametoa kauli hiyo leo ofisini kwake alipozungumza na waandisha wa habari kuhusu zuio la mkutano wa Chadema uliopangwa kuanza leo katika wilaya ya Mufindi.

" Nawatangazia wanasiasa na vyama vyote vya siasa pamoja na wananchi wa mkoa wa Iringa kuwa hakutakuwa na mikutano ya kisiasa kutokana na shughuli za sensa zinazoendelea ....hivyo basi nawaomba wananchi wote kutoshiriki mikutano yoyote ya kisiasa itakayoitishwa na wanasiasa "alisisitiza

Kuwa mikutano hiyo imezuiliwa kwa kipindi hiki cha sensa kilichoongezwa hadi hapo tamko litakapotolewa tena na msajili wa vyama vya siasa John Tendwa kama alivyokwisha kutoa tamko la kuzuia shughuli hizo za vyama vya siasa kwa kipindi hiki cha sensa.

"Wananchi wote wa mkoa wa Iringa mnaombwa kutii sheria bila shuruti hii ni amri ....nawaombeni sana wananchi kutodanganywa na wanasiasa kwa kuvunja sheria "aliongeza kamanda huyo wa polisi.

Hata hivyo alisema kuwa kimsingi zoezi la sensa lilipaswa kuhitimishwa Septemba mosi mwaka huu ila kutokana na serikali kuongeza muda wa zoezi hilo bado jeshi hilo la polisi linazingatia maagizo ya Msajili wa vyama vya siasa kama alivyoyatoa kwa jeshi hilo.

Kamanda Kamuanda alisema kuwa jeshi hilo la polisi wala msajili wa vyama vya siasa hajazuia vyama vya siasa kuendelea na vikao vyao vya ndani kwa kipindi hiki na kuwa hata Chadema wakiwa mkoani Iringa wameendelea kufanya vikao vyao vya ndani katika kata mbali mbali za mkoa wa Iringa na hakuna mtu aliyewazuia kuendelea kufanya hivyo.
Majibu ya Dkt Slaa
Wakati jeshi la polisi likipinga shughuli hizo za vyama vya siasa kufanya mikutano ya hadhara katibu mkuu wa Chadema Taifa Dkt Willbroad Slaa ameibuka na kusema kuwa chama chake kitaendelea na mikutano kama kilivyojipangia na kuwa wapo tayari kwa lolote litakalojitokeza .

Dkt Slaa alisema kuwa walivumilia mara ya kwanza walipozuiwa mikutano hiyo mkoani Iringa na kuvuta subira hadi jumamosi zoezi hilo lilipomalizika sasa anashangazwa kuona jeshi hilo likiendelea kuzuia mikutano hiyo tena.

"Tumemsikiliza kamishina wa sensa Hajati Amina Mrisho Said kuwa hadi sasa watu asilimia 95 wameandikishwa huku akiwata wale ambao bado kuwapigia simu wenyeviti wa mitaaa na vijiji ili wakaandikishwe na makarani wa sensa ....sasa jeshi la polisi linataka kutuambia kuwa hao watu asilimia 5 waliobaki wapo Iringa peke yake hadi wakazuia mikutano yetu? tunasema hatutakubali tutaendelea na mikutano yetu kama kawaida hatupotayari kabisa kusubiri hadi tarehe nane" alisema Dkt Slaa.

Pia alisema kuwa kama ni uzalendo sasa umefika kikomo na kuwa wataendelea na ratiba zao za mikutano kama ilivyopangwa na watapambana kwa lolote .
MWISHO

4 comments:

Anonymous said...
nashauri kuwa kwa ajili ya uhai wa Watanzania bwana Slaa asitishe mikutano hadi hapo tarehe nane, sioni kama kuna faida kuacha familia zinateseka miaka yooote baadae kwa kuuawa wapendwa wao kama Daudi Mwangosi kuliko kusubiri hadi hiyo muda ifike, kwani kuna tofauti gani jamani??? halafu jeshi letu la polisi kwa nini linajenga uadui na wananchi?? kuna haja gani kutumia silaha kubwa hivyo kama mabomu kwa wananchi wasio na kitu? Wasingewatawanya wangesubiri mkutano uishe halafu hao viongozi wa chadema wakamatwe wawekwe ndani au wawajibishwe kwa namna yoyote ile.
Lear said...
Tatizo la mapolisi ni kutafuta kupandishwa madaraja! Pole kamuhanda umenuka kuliko kinyesi
Anonymous said...
Kwa taarifa zilizopo ule haukuwa mkutano, bali ilikuwa ni ufunguzi wa Tawi la CHADEMA la pale Nyololo, watu wenyewe walikuja baada ya kupata taarifa kuwa Katibu Mkuu wa CAHDEMA anakuja kufungua tawi pale. Hivyo CHADEMA wasilaumiwe kwa hilo, lakini ajabu mbona mikutano ya CCM inafnayika wakati huu pia ?

Huu msimamo ukoje? Kunafichwa nini hapa?

Bernard Rwebangira said...
Inasikitisha sana, kwamba kuna baadhi ya watu wanadhani wakiwa katika magwanda hayo wana tiketi ya kuishi milele! na hivyo kwao ni sawa tu kukatisha maisha ya watu wengine?
naamini malipo ni hapahapa duniani, kumwaga damu isiyo na hatia ata kama weye ni mwabudu shetani utalipa hapahapa.
RIP Daudi Mwangosi