Pichani
ni Ndugu Absalom Kibanda akiwa amelazwa kwenye moja ya chumba cha
matibabu,hospitali ya Taifa Muhimbili.Get Well soon Absalom Kibanda.Picha kwa hisani ya Mtandao wa Mabadiliko.
Mwenyekiti
wa Jukwaa la wahariri,na Mhariri Mkuu wa Mtendaji wa New Habari
Coperations Ltd, Ndugu Absalom Kibanda, amevamiwa usiku wa kuamikia leo
akiwa anashuka nyumbani kwake Mbezi Beach na watu wasiofahamika na
kumpiga kichwani. Amepata majeraha Makubwa kichwani na hasa
jichoni,aidha taarifa inaeleza kuwa baada tukio hilo Kibanda alikimbizwa
hospitali ya Taifa Muhimbili kwa Matibabu.
Wadau
hii ni taarifa ya kushtua sana,lakini tutazidi kutaarifiana kadiri ya
habari zitakavyokuwa zinapatikana,kikubwa tumwombee Mungu amponye haraka
mpiganaji mwenzetu.