Wednesday, December 4, 2013

TAZAMA HAPA NYIMBO 50 ZA BONGO FLAVA ZILIZOSIKILIZWA ZAIDI MTANDAONI MWAKA 2013




Zimebaki siku 26 tu hadi tuumalize mwaka 2013. Kwa kutumia akaunti maarufu za mtandao wa hulkshare zinazomilikiwa na blog tano nchini Tanzania, Bongo5 imeandaa orodha ya nyimbo zilizosikilizwa zaidi kwenye mtandao mwaka 2013. Blog hizo ni pamoja na Bongo5, Gongamx, Dj Choka, Sam Misago na Hass Baby. Pamoja na Hulkshare ndio website ya kuhifadhia nyimbo mtandaoni maarufu zaidi kuliko yote kwa sasa.

Hii ni orodha kamili ya nyimbo 50 zilizosikilizwa zaidi mtandaoni mwaka 2013.

1.Nay wa mitego ft Diamond Platnumz – Muziki Gani
14 Mar 2013
Imesikilizwa mara 93,895
Imepakuliwa mara 34,949

2.Young Killer ft Stamina & Quick Rocka – Jana na Leo

25 Apr 2013
Imesikilizwa mara 79,100
Imepakuliwa mara 31,175

3.Ben Pol – Jikubali
2 May 2013
Imesikilizwa mara 76,424
Imepakuliwa mara 30,397

4.Lady JayDEE – Yahaya

12 Jun 2013
Imesikilizwa mara 75,764
Imepakuliwa mara 12,846


5.Ney wa Mitego ft. Neyba – Salam Zao
31 Jul 2013
Imesikilizwa mara 64,062
Imepakuliwa mara 18,313


6.Diamond Platnumz- Mapenzi Basi
12 Apr 2013
Imesikilizwa mara 52,255
Imepakuliwa mara 21,589


ENDELEA KUTIZAMA NYIMBO ZAIDI KWA KUBOFYA HAPA CHINI


7.Rama Dee Ft Lady Jaydee – Kama Huwezi
3 Jul 2013
Imesikilizwa mara 52,096
Imepakuliwa mara 8,190


8.Ommy Dimpoz ft J Martins – Tupogo
1 Aug 2013
Imesikilizwa mara 47,100
Imepakuliwa mara 9,059

9.Izzo B Ft Barnaba Na Shaa – Love Me

30 Apr 2013
Imesikilizwa mara 46,151
Imepakuliwa mara 15,630


10.Chege ft Malaika- Uswazi Take Away
4 Feb 2013
Imesikilizwa mara 45,307
Imepakuliwa 23,411

11.Shetta Ft Rich Mavoko – Sina Imani

29 Mar 2013
Imesikilizwa mara 43,299
Imepakuliwa mara 16,105


12.Rich Mavoko – Roho Yangu
18 Sep 2013
Imesikilizwa mara 42,778
Imepakuliwa mara 3,330


13.Jux – Uzuri Wako
13 Mar 2013
Imesikilizwa mara 39,224
Imepakuliwa mara 14,139


14.Blue – Pesa
4 Sep 2013
Imesikilizwa mara 38,094
Imepakuliwa mara 3,908


15.Roma – 2030
4 Jan 2013
Imesikilizwa mara 37,841
Imepakuliwa mara 19,161


16.Stamina ft. Fid Q – Wazo La Leo
11 Jan 2013
Imesikilizwa mara 36,783
Imepakuliwa mara 19,127


17. Diamond Platnumz – Number 1
Imesikilizwa mara 33,707
Imepakuliwa mara 3,827


18.Cassim Mganga – I Love you
4 Jul 2013
Imesikilizwa mara 33,267


19. Quick Rocka ft. Ngwair & Shaa – My Baby
21 Jun 2013
Imesikilizwa mara 32,517
Imepakuliwa mara 10,791

20.Nikki Mbishi – Ney Wa Mitego
8 May 2013
Imesikilizwa mara 31,734
Imepakuliwa mara 11,521

21.Vanessa Mdee – Closer

Jan 2013
Imesikilizwa mara 27,838
Imepakuliwa mara 15,264


22.MwanaFA & AY Ft J Martins – Bila Kukunja Goti
26 Jun 2013
Imesikilizwa mara 27,715
Imepakuliwa mara 8,699


23.Young Killer ft Bright & Nemo – Mrs Super Star
2 Aug 2013
Imesikilizwa mara 26,664
Imepakuliwa mara 4,117


24.Lady Jaydee ft. Prof. Jay – Joto Hasira
7 Mar 2013
Imesikilizwa mara 26,316
Imepakuliwa mara 10,964

25.Linex Ft. Sunday – Kimugina

2 Aug 2013
Imesikilizwa mara 25,829

26.Nikki wa Pili ft Joh Makini – Bei ya Mkaa
30 Jul 2013
Imesikilizwa mara 24,476
Imepakuliwa mara 5,477

27.Nikki Wa Pili – Nje ya Box
15 Feb 2013
Imesikilizwa mara 20,819
Imepakuliwa mara 8,844

28.Kala Jeremiah Ft Ben Pol – Karibu Dar
13 Mar 2013
Imesikilizwa mara 20,437
Imepakuliwa mara 6,254

29.Nikki Mbishi & Godzilla Feat. Cliff Mitindo – Kill yoself
4 Feb 2013
Imesikilizwa mara 20,128
Imepakuliwa mara 12,145

30. Snura – Nimevurugwa
29 Jul 2013
Imesikilizwa mara 20,078
Imepakuliwa mara 4,780

31. Stamina ft Darasa, Warda – Mwambie Mwenzio

25 Jul 2013
Imesikilizwa mara 17,723
Imepakuliwa mara 6,244

32.Linah- Tumetoka Mbali

20 Aug 2013
Imesikilizwa mara 17,747
Imepakuliwa mara 3,438

33.Suma Mnazaleti ft Tunda – Tuko wangapi
13 Mar 2013
Imesikilizwa mara 17,630
Imepakuliwa mara 7,381

34. Madee – Sio Mimi
Imesikilizwa mara 17,411
Imepakuliwa mara 8,043


35.Ben Pol ft Alice – Waubani

8 Sep 2013
Imesikilizwa mara 17,268
Imepakuliwa mara 3552

36.Recho – Umependeza
4 Sep 2013
Imesikilizwa mara 16,894
Imepakuliwa mara 4,211

37.Lucci & Julio ft Jokate – Waters Up
2 Feb 2013
Imesikilizwa mara 16,686
Imepakuliwa mara 34,271

38.Gosby – BMS ( Baby Making Swag)

28 Jun 2013
Imesikilizwa mara 16,492
Imepakuliwa mara 3,886

39.Gosby – Monifere

9 Oct 2013
Imesikilizwa mara 16350
Imepakuliwa mara 2,626

40.Nyandu ft Young Killer, Young D & Belle 9 – Kwa Mafans
3 Jul 2013
Imesikilizwa mara 16,202
Imepakuliwa mara 6,629

41.Hard Mad – Naishi Gheto

10 Nov 2013
Imesikilizwa mara 15,573

42.Izzo B ft Ngwair and Quick Rocka – Ball Player
23 Jan 2013
Imesikilizwa 15,258
Imepakuliwa mara 8659

43.Young Dee ft Mr. Blue – Hujali
29 Jan 2013
Imesikilizwa mara 15,285

44.Suma Mnazareti Ft Richard – Umechelewa
20 Sep 2013
Imesikilizwa mara 15,052
Imepakuliwa mara 2,068

45.Mahakama ya Mapenzi – Linex.mp3

28 Jan 2013
Imesikilizwa mara 15,048
Imepakuliwa mara 9,158

46.Sajna ft. Ben Pol & Sisa Madini – Ningekuwa Single
10 Jul 2013
Imesikilizwa mara 14,463
Imepakuliwa mara 2,208

47.Bob Junior ft Vanessa Mdee – Bashasha
Imesikilizwa mara 13,792
Imepakuliwa mara 2,131

48.Chid Benz-Nakaza Roho
14 Aug 2013
Imesikilizwa mara 13,673
Imepakuliwa mara 2,439

49.Diamond – Kama Nikifa Kesho

7 Oct 2013
Imesikilizwa mara 13,542
Imepakuliwa mara 4,009


50. Cindy Rulz ft. Dunga – Let’s Wait

31 Oct 2013
Imesikilizwa mara 12,529
imepakuliwa mara 936

Bonus

51. Fid Q ft Juma Nature – Siri ya Mchezo-
19 Oct 2013
Imesikilizwa mara 10,929
Imepakuliwa mara 724

52. T.I.D Ft Kassim na Mr Blue – Tamu Asali
20 Sep 2013
Imesikilizwa mara 10,906
Imepakuliwa mara 1,866


53. Mabeste ft Peter Msechu – NISHAURI

7 Aug 2013
Imesikilizwa mara 10,692
Imepakuliwa mara 3,272

SOMA JACK WALIPER ALIVYOFUNGUKA YA MOYONI NAKUANIKA A DALASS NA KUKIRI KUWA ALI KIBA NDIO ALIYEMFUNZA MAPENZI


MOYO; 
huhifadhi mengi mazito hasa ya kuumiza! Staa mkubwa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe amejikuta akimwaga machozi wakati akianika siri tano nzito kuhusu mapenzi katika mahojiano (exclusive interview) 


Katika ‘intavyu’ hiyo iliyofanyika Jumatatu iliyopita kwenye Ofisi za Global Publishers, Bamaga-Mwenge jijini Dar kuanzia saa 8:44 alasiri hadi saa 10:44 jioni, Wolper alifunguka vitu vingi.

KISA/MKASA
Akizungumza kwa masikitiko, uchungu na majuto, Wolper alisema hawezi kumsahau mwanaume huyo ambaye ni Abdallah Mtoro ‘Dallas’ kwa namna alivyomwingia kijanja na kutaka kumvunjia heshima aliyoijenga karibia miaka kumi nyuma.


ALIANZIA WAPI NA DALLAS?
“Siku ya kwanza Dallas alinipigia simu na kuniambia aliniona Magomeni (Dar). Naikumbuka sana siku hiyo, ilikuwa baada ya mizunguko yangu, mwanzoni sikupokea simu yake kwa sababu ilikuwa namba ngeni kwangu.
“Nilimsikiliza sana. Jamani yule mwanaume anaongea kwa ushawishi wa hali ya juu mno. Nilishangaa aliponieleza kila kitu kuhusu familia yangu na nyumbani kwetu. Kumbe tayari alishaunda urafiki na baba yangu (mzee Massawe).

“Mwanzoni nilidhani ni tapeli. Nikamkatia simu. Akaendelea kunipigia na nilipoona imekuwa kero kubwa nilipokea. Ili kuthibitisha anawajua wazazi wangu, alinitajia namba zao za simu ambazo ni za kweli.
“Pamoja na hilo nilimfanyia nyodo, si unajua mtoto wa kike? Lakini aliniongelesha kwa upole hadi nikapunguza nyodo zangu.

“Aliniuliza nataka anifungulie biashara gani. Nikamwambia biashara ya nguo. Akaniuliza nataka mtaji kiasi gani. nikamwambia dola laki moja kwa sababu nilikuwa sitaki fremu moja, nilitaka nyumba nzima. Akaniambia hakuna tatizo.
“Pia aliniuliza naishi wapi? Nikamwambia Sinza (Dar) alionesha dharau kwenye simu akaniambia atanihamishia Mbezi Beach.

“Aliniuliza natembelea gari gani? Nikamwambia Toyota Noah. Akaniambia ningependa aninunulie gari gani? Nikamjibu Toyota Discovery lakini yeye akasema ataninunulia Toyota Harrier.

“Kweli baada ya siku mbili-tatu nililetewa Toyota Harrier nyeusi nyumbani. Niliogopa isijekuwa mtego nikaingia kwenye matatizo hivyo nilimzungusha mtu aliyeniletea hadi Sinza-Mori nikamwambia apaki kwenye kituo cha teksi, nikaenda na dereva nikalichukua hadharani ili lolote likitokea nipate msaada.

“Nilikabidhiwa funguo za lile gari na documents zake, nikaondoka nalo hadi nyumbani kwangu. Kesho yake Dallas alimtuma mtu aniletee dola za Kimarekani 15,000 (zaidi ya Sh. milioni 24). Nilipouliza za nini aliniambia ni kwa ajili ya shopping ya kutembelea Harrier niachane na zile swaga za kwenye Noah (fedha inaongea). Kisha akanitumia cheni ya dhahabu.

“Siku iliyofuata alinitumia Sh. milioni 15 nipeleke nyumbani nikawaambie wazazi nimepata mchumba ambaye angeenda kujitambulisha baadaye. Niliwaambia ni Dallas ambaye walikiri kumfahamu kwa sababu alishawapigia simu na kujitambulisha kuwa ni mkwe wao.”

AMESHAKUTANA NA DALLAS?
“Hadi hapo nilikuwa sijamuona Dallas kwa sura na fedha nilikuwa natumiwa kila siku.
“Wakati hayo yakiendelea akaagiza nihamishiwe Mbezi Beach na kununuliwa lile gari lililoibua mzozo BMW X6.
“Nakumbuka siku niliyokabidhiwa lile gari nililia sana. Sikuamini macho yangu kwa sababu Dallas aliniambia amenitumia kazawadi kumbe ni BMW X6 (lina stori ndefu inakuja)!

“Kumbuka mwanzoni nilikuwa na boyfriend ambaye tulipendana sana lakini hatukupanga kufunga ndoa. Nilimweleza kila kitu akakubaliana na mimi japokuwa aliumia.
“Maskini! Kuanzia hapo nikawa nimeachana na yule boyfriend wangu lakini hakukuwa na namna kwa sababu niliamini nimepata mchumba wa kunioa.

ATAKIWA KUBADILI DINI
“Baadaye Dallas aliniambia nimeshakuwa mchumba wake hivyo nibadili dini. Kweli nilibadili nikawa Muislam na jina langu likawa Ilham. Hicho kilikuwa kipindi kigumu sana maishani mwangu kwa sababu nilionekana ni muasi katika dini yangu ambayo mama ni mzee wa usharika na mwimba kwaya, baba ni mtu wa kanisani sana.”

NINI KILIFUATA?
“Siku moja nilikuwa Tanga nashuti filamu, nilikuwa nikitoka hapo niende Morogoro. Dallas alinipigia simu akaniambia yupo Nairobi (Kenya) anakuja Tanzania. Nilimwambia nipo Tanga akaniambia atanifuata kule. “Niliendelea kupiga mzigo. Zilipita saa nyingi, baadaye nikiwa na kruu yangu, Dallas alinipigia simu akaniambia ameniona.
“Nilikataa, akaniambia namna nilivyo, nguo nilizovaa na watu niliokuwa nao, alipatia. Kumbe alikuja na Toyota Prado.

WOLPER MORO, DALLAS DAR
“Tulipomaliza kurekodi Tanga tulikwenda Morogoro, yeye aliniambia anaelekea Dar. Tulikuwa tunawasiliana. Nilipomaliza kurekodi Moro nilirejea Dar. Hapo ndipo vituko vikawa juu ya vituko.

“Niliambiwa mara kaonekana sehemu akiwa na mwanamke au wanawake. Mimi sikujali kwa sababu nilipomuuliza aliniambia hatuwezi kuonana kwa sababu kipindi hicho alikuwa katika swaumu hivyo akionana na mimi nitamharibia. (ulikuwa mwezi mtukufu).

BADO HAWAJAKUTANA?
“(Mguno) Hapo bado hatujakutana lakini yupo mjini na amejaa tele kwenye kumbi za starehe.
“Baada ya kumaliza swaumu, siku moja aliniambia anakuja nyumbani Mbezi Beach. Niliwaalika marafiki zangu tukapika vyakula, tukafanya usafi na kufukiza udi chumbani. Nilitandika mashuka meupe kitandani na kujipara kisha nikavaa ushungi kuanzia mchana nikakaa kama malkia nikimsubiri mchumba.

“Huwezi amini, hadi giza linaingia Dallas hakutia mguu. Nilipataje aibu kwa rafiki zangu waliotaka kumuona huyo mchumba? Ninyi acheni tu!
“Nilipomuuliza aliniambia alipata dharura kuna biashara alikuwa anafanya

HATIMAYE WAKUTANA LAKINI…
“Nilikasirika sana, nikasema huyu ni mchumba gani asiyetaka kuja kwangu? Nikampa muda wa siku tatu aje nyumbani na alete nguo zake zote. Kweli, siku ya tatu,  asubuhi nilimsikia mtu akiita ‘Ilham Wolper Dallas’. Nilishajua sauti yake kupitia simu hivyo nilimkaribisha na nguo zake nikaingiza ndani. Lakini cha kushangaza alikuja na pikipiki!

“Alishinda nyumbani siku hiyo maana kuna ndugu zake walikuja. Hatukufanya chochote. Dallas aliishia kunibusu shavuni kisha jioni akaondoka.
“Mjini kukawa hakukaliki. Natumiwa picha akiwa na wanawake tofautitofauti. Mmoja wa wanawake hao niliambiwa eti ana ‘ngoma’! Jamani hii dunia ina kichaa!

“Muda ukasonga, vitimbi vikawa vingi. Dallas simuoni. Muda wa kukaa kwenye ile nyumba uliisha hivyo nikahama na nikamwambia akachukue nguo zake.

UCHUMBA WAVUNJIKA, SASA ANAPUMZIKA HAPA
“Baadaye uchumba ukavunjika tena mimi ndiyo nilimwambia simtaki tena. Nilikaa muda hadi baadaye nilipopata mwanaume wangu wa sasa. Anani-control vizuri kwa sababu kanipita umri na ana busara. Tunapendana sana. Najuta kumfahamu Dallas. Siwezi kusahau tukio hilo katika maisha yangu. Dallas alicheza na hisia za moyo wangu. (akaangua kilio) Niliteseka sana. Ni Mungu tu anajua…

VIPI KURUDIA UKRISTO?
“Nimekaa muda siendi kanisani. Nilikuwa najifungia ndani nalia kama mama yangu alivyokuwa anafanya. Siku moja nilimwambia mwanaume wangu akaniambia kuliko kulia kila siku bora nirudi kanisani. Ndipo nikarudia ukristo. Kwa sasa nasali Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Kijitonyama, Dar,” alisema.

MBALI NA DALLAS
Kwa mara ya kwanza Wolper alikubali kuorodhesha listi ya wanaume aliowahi kuwa nao kimapenzi kwa kuwachambua mmoja mmoja.

ALI KIBA
Bila kupepesa macho, Wolper alikiri kuwa msanii wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba ndiye aliyemfundisha mapenzi: “Ni kitambo kidogo. Wote hatukuwa mastaa lakini yeye alifanikiwa kuchomoka. Kabla ya Ali (Kiba) nilikuwa na mwanaume lakini hatukuduu kwa maana ya utu uzima, ilikuwa yale ya kitoto. Lakini Ali ndiye hasa aliyeniingiza kwenye ulimwengu wa mapenzi.

KWA NINI WALIACHANA?
“Ali akawa staa. Alipokwenda nje nikasikia wanawake wanamshobokea. Sasa mimi sikutaka karaha nikakaa pembeni lakini jamaa ni mtu poa sana na tukikutana tunasalimiana freshi kabisa.”

DIAMOND VIPI?
“Ni kweli niliwahi kuwa na Diamond (msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul). Tulikuwa na uhusiano lakini pia alikuwa mshirika wa kibiashara (hataki kuitaja). Yeye alikuwa hawezi kulala bila kuniona, lakini tulikaa kama mwezi mmoja, kwa sasa amebaki kuwa rafiki yangu na siyo mpenzi tena kama zamani,” alisema Wolper.

VIPI KUHUSU JUX?
“Jux (msanii wa Bongo Fleva, Juma Khalid) nilikuwa naye kabla ya Dallas na yule mwanaume wangu niliyeachana naye wakati wa Dallas. Katika maisha yangu nilimpenda sana Jux. Siyo marioo ni mwanaume mtafutaji aliyejiamini. Kwa sasa sipo naye. Dallas pia alichangia mimi kuachana na Jux,” alimalizia Wolper ambaye kwa sasa ana mwanaume asiyependa kumwanika.

HII NDIZO PICHA 11 ZINAZOONESHA HALI HALISI YA MITAA MBALIMBALI YA JIJI LA DAR BAADA YA MVUA KUNYESHA



ENDELEA KUTIZAMA PICHA ZAIDI KWA KUBOFYA HAPA CHINI